Kampuni ya China kujenga kituo cha umeme nchini Sudan
2022-12-26 08:53:01| CRI


 

Kampuni ya China XD Group imesaini makubaliano na serikali ya Sudan ya kujenga kituo cha umeme huko Al-Fula, mji mkuu wa Jimbo la Kordofan Magharibi nchini Sudan, ili kuunganisha miji ya jimbo hilo na gridi ya taifa ya umeme.

Waziri wa Fedha wa Sudan Jibril Ibrahim, wawakilishi wa Ubalozi wa China nchini Sudan na maafisa kutoka Jimbo la Kordofan Magharibi walihudhuria hafla ya utiaji saini katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Ibrahim amesema katika mkutano wa viongozi wa China na nchi za Kiarabu uliofanyika hivi karibuni huko Riyadh, China iliahidi kupanua uhusiano wake na Sudan, na anatumai kuwa uhusiano huu utasaidia kuendeleza miundombinu ya Sudan na kupata maendeleo katika nyanja mbalimbali. Ibrahim ameongeza kuwa ushirikiano kati ya Sudan na China unatoa matokeo.

Kwa upande wake, kansela wa kibiashara wa Ubalozi wa China nchini Sudan Guohu ameahidi kuendelea kuhimiza makampuni ya China kuwekeza nchini Sudan.