UM na washirika wake wa kimataifa wana wasiwasi juu ya kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa Sudan Kusini
2022-12-29 08:54:01| CRI


 

Umoja wa Mataifa na washirika wake duniani Jumatano walielezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa ghasia katika eneo la Utawala la Greater Pibor mashariki mwa Sudan Kusini zinazofanywa na vijana wenye silaha kutoka Jimbo la Jonglei.

Kwenye taarifa yao ya pamoja iliyotolewa mjini Juba, Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Tume ya Umoja wa Afrika nchini Sudan Kusini, Umoja wa Ulaya, na vyombo vingine vya kikanda vimezitaka pande zinazohusika kusitisha mapigano mara moja, kujizuia, na kuheshimu haki za binadamu.

Wamesema wakati jukumu la msingi la kulinda raia ni la Serikali ya Mpito ya Sudan Kusini, UNMISS na washirika wake wako tayari kutoa msaada wote muhimu ili kulinda raia katika maeneo yaliyoathiriwa, na kutoa wito kwa viongozi wa Sudan Kusini kuingilia kati haraka ili kusitisha mapigano na kuhakikisha usalama wa raia pamoja na upatikanaji usio na kipingamizi wa misaada ya kibinadamu kwa watu walioathiriwa na mapigano.