China yashika nafasi ya juu katika utafiti wa UM kuhusu huduma za serikali mtandaoni
2022-12-29 08:53:19| CRI


 

China imeshika nafasi ya 43 kati ya nchi 193 katika maendeleo ya huduma za serikali mtandaoni mwaka 2022, kutoka nafasi ya 78 mwaka 2012.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (DESA), China imekuwa moja ya nchi zilizoshuhudia uboreshaji mkubwa katika suala la viwango vyake vya huduma za serikali mtandaoni. Toleo la lugha ya Kichina la utafiti huu lilitolewa siku ya Jumatano kwa ushirikiano wa UN DESA na kituo cha utafiti cha huduma za serikali mtandaoni kilicho chini ya Chuo cha Chama cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China.

Kielezo cha Maendeleo ya Huduma za Serikali Mtandaoni nchini (EGDI) kimekuwa 0.8119 katika mwaka huu wa 2022, kikiwa juu kuliko thamani ya wastani duniani ambayo ni 0.6102, na kuiweka China katika kundi la juu sana la EDGI.