Kuanzishwa kwa kituo cha RMB nchini Mauritius kwahimiza biashara kati ya China na Afrika
2022-12-29 08:52:17| CRI


 

Tawi la Benki ya China nchini Mauritius hivi karibuni lilifanya hafla ya uzinduzi wa huduma ya Renminbi (RMB) huko Port Louis, mji mkuu wa Mauritius. Wataalam wa China na Mauritius wamesema kuanzishwa kwa kituo hicho si kama tu kutanufaisha biashara kati ya China na Mauritius, bali pia kutahimiza maendeleo ya biashara kati ya China na Afrika.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Mabenki la Mauritius Daniel Esso, amesema kuanzishwa kwa kituo cha huduma za RMB nchini Mauritius kuna manufaa kwa mazingira ya biashara nchini Mauritius, barani Afrika na hata duniani kote. Ameongeza kuwa kuanzishwa kwa kituo hicho si kama tu kutarahisisha biashara kati ya Mauritius na China, bali pia kutapunguza gharama za biashara kwa kiasi kikubwa, na zaidi ya hayo, kituo hicho kitaiwezesha Mauritius kuunganisha mifumo tofauti ya kifedha duniani.

Mkuu wa tawi la Benki ya China nchini Mauritius Li Lianhong amesema katika miaka kumi iliyopita, China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika, na baada ya kuanzishwa kwa kituo cha huduma za RMB, Mauritius inaweza kuwa daraja la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya Afrika na China, na hata kati ya Afrika na Asia.