Watu wasiopungua 19 wafariki katika ajali ya moto nchini Kambodia
2022-12-30 09:21:45| cri

Watu wasiopungua 19 jana walifariki katika ajali ya moto mkubwa ulioteketeza hoteli moja huko kaskazini magharibi mwa mkoa wa Banteay Meanchey nchini Kambodia.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, watu wengine 23 walijeruhiwa vibaya na wengine 50 walipata majeraha madogo katika ajali hilo. Zaidi ya wafanyakazi 360 wa dharura, wakiongozwa na mkuu wa Polisi wa mkoa wa Banteay Meanchey Meja Jenerali Sithi Loh, walijiunga na kazi za uokoaji wakitumia magari 11 ya kuzima moto ili kukabiliana na moto huo.