Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa gesi nchini Afrika Kusini yapanda na kufikia 27
2022-12-30 09:13:49| CRI


 

Ofisa wa Idara ya Afya ya mkoa wa Gauteng nchini Afrika Kusini Bw. Motalatale Modiba jana alithibitisha kuwa, hadi kufikia tarehe 29, mlipuko wa lori lililobeba gesi uliotokea tarehe 24 mwezi Desemba huko Boksburg umesababisha vifo vya watu 27, wakiwemo wafanyakazi 10 wa afya.

Wafanyakazi hao 10 wa afya kwenye hospitali ya Tambo Memorial, ambayo iko mita 100 kutoka eneo la mlipuko, walikufa kwenye mlipuko huo, na wengine watatu wako mahututi hospitalini.