Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok ajiuzulu
2022-01-03 08:28:58| CRI

Waziri mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok jana Jumapili alitangaza kujiuzulu wadhifa wake kufuatia msukosuko wa kisiasa unaotokea nchini humo.

Akiwahutubia wananchi kupitia televisheni ya Sudan, Bw. Hamdok amesema kutokana na tofauti kati ya vyama vya kisiasa na mgogoro kati ya pande zote za mpito, juhudi alizozifanya kwa lengo la kufikia mwafaka ili kutimiza ahadi yake ya kuleta usalama, amani na haki na kukomesha umwagaji damu, zote zimeshindwa.

Bw. Hamdok amesisitiza umuhimu wa kuanzisha mazungumzo ya pande zote ili kumaliza mgororo wa kisiasa nchini humo.

Habari nyingine zinasema waandamanaji wawili wameuawa kwa kupigwa risasi kichwani kwenye maandamano yaliyotokea jana mjini Khartoum, na kufanya idadi ya vifo kutokana na mgogoro huo ifikie 56 tangu Oktoba 25 mwaka 2021.