Polisi wa Kenya waanzisha msako baada ya mauaji ya watu sita mkoani Pwani
2022-01-04 08:44:08| CRI

Vyombo vya usalama vya Kenya vimeanzisha msako mkali wa wapiganaji takribani 80 wa kundi la al-Shabaab waliowaua watu sit katika mji wa pwani wa Lamu.

Mkuu wa kaunti ya Lamu Bw. Irungu Macharia amesema watuhumiwa ni wapiganaji wa kundi la al-Shabaab na uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea, na maofisa wa jeshi la Kenya, polisi na kikosi cha kupambana na ugaidi wamefika kwenye eneo la tukio.

Amesema wanashuku kuwa wapiganaji wa al-Shabaab ndio waliofanya mauaji, lakini bado wanachunguza wasifu wao na nia ya mauaji.

Wenyeji wa Lamu wamesema kumekuwa na ripoti kuhusu ongezeko la uwepo wa wapiganaji wa kundi la al-Shabaab katika mji wa Lamu, hasa katika msitu wa Boni, ambao unatumika kama maficho na mapumziko ya wapiganaji hao, baada ya kufanya mashambulizi katika baadhi ya maeneo ya Lamu na mengine kwenye mpaka na Somalia.