Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan asisitiza kuundwa serikali huru
2022-01-04 09:17:17| CRI

Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan amesisitiza umuhimu wa kuunda serikali huru.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan, Bw. Al-Burhan amesema hayo kupitia taarifa iliyotolewa kwa maofisa wa jeshi la Sudan na Kikosi cha Uungaji Mkono wa Kasi katika makao makuu ya jeshi hilo huko Khartoum.

Amesisitiza kuwa umuhimu wa kutimiza majukumu ya kipindi cha mpito, ikiwa na kipaumbele cha kutimiza amani, usalama na kufanya uchaguzi. Bw. Al-Burhan ameahidi kuwa jeshi litalinda mpito wa kidemokrasia hadi utakapofanyika uchaguzi huru na wa haki.

Wakati huohuo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani mabavu yanayoendelea dhidi ya waandamanaji nchini Sudan, huku akitoa wito kwa kikosi cha usalama cha Sudan kujizuia na kuzingatia wajibu kuhusu uhuru wa kuandamana na kujieleza.