Somalia yaanza mazungumzo ya kitaifa kuhusu usalama na uchaguzi ulioahirishwa
2022-01-04 08:46:24| CRI

Waziri mkuu wa Somalia Mohamed Roble jana Jumatatu alianza mazungumzo ya kitaifa yanayolenga kuharakisha mchakato wa uchaguzi ulioahirishwa.

Ofisi ya Waziri Mkuu imesema mkutano huo uliwaleta pamoja marais kutoka majimbo ya Jubbaland, HirShabelle, SouthWest, Puntland, Galmudug and Banadir, na unafuatilia masuala ya usalama na kukamilisha uchaguzi wa bunge.

Mkutano huo umekuja kufuatia mvutano unaotokana na uchaguzi na tuhuma za ufisadi, baada ya rais Mohamed Farmajo kujaribu kumsimamisha kazi Bw. Roble.