Rais wa Msumbiji na mke wake wathibitishwa kuambukizwa COVID-19
2022-01-04 09:12:17| CRI

Ofisi wa rais wa Msumbiji jana usiku ilitangaza kuwa rais Filipe Nyusi na mkewe Bibi Isaura Nyusi wamegunduliwa kuambukizwa COVID-19.

Taarifa imesema Rais Nyusi na mkewe hawakuwa na dalili, matokeo ya vipimo vya kawaida vya jana alasiri yameonesha kuwa wameambukizwa virusi hivyo na sasa wako karantini.

Rais Nyusi alifanya shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea maeneo tofauti, na kufanya mikutano na wajumbe kadhaa wa taifa katika siku za mwisho wa mwaka jana.

Kwa kuzingatia kanuni za afya, licha ya kuwa hana dalili, rais Nyusi na mkewe walichukua uamuzi wa haraka wa kujiweka karantini, wakati wakisubiri matokeo ya uhakika ya kipimo cha PCR.