Polisi wa Kenya wakamata watuhumiwa watano wa mauaji ya watu 7
2022-01-05 09:26:26| cri

Polisi wa Kenya wamesema wamewakamata watuhumiwa watano wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya raia saba yaliyotokea Jumatatu kwenye eneo la Widhu Majembeni na Bobo-Sunkia huko Lamu.

Msemaji wa Polisi ya Kenya Bw. Bruno Shioso, amesema watuhumiwa hao wanahojiwa kuhusu mashambulizi hayo yanayohusu mgogoro wa ardhi huku uchunguzi husika ukiwa umeanzishwa ili kuthibitisha kama mashambulizi hayo yanahusiana na wapiganaji wa kundi la al-Shabab au wenzi wao.

Katika miaka ya hivi karibuni kaunti ya Lamu imekuwa sehemu nyeti kutokana na mashambulizi makali yanayofanywa na wanamgambo ambayo husababisha vifo vingi vya maafisa wa usalama na raia.