Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan asema anataka kumaliza mgogoro wa kisiasa kupitia mazungumzo
2022-01-05 09:12:56| CRI

Mwenyekiti wa baraza la utawala la Sudan Bw. Abdel Fattah Al-Burhan amesema, mlango wa mazungumzo uko wazi kwa pande zote za kisiasa uko wazi, ili kumaliza mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na baraza hilo, Bw. Al-Burhan amesema hayo wakati alipokikutana na balozi mdogo wa Marekani huko Khartoum Bw. Brian Shukan katika ofisi yake.

Amesisitiza haja ya kuendelea kufanya mazungumzo kati ya pande mbalimbali ili kufikia makubaliano ya pamoja ya taifa juu ya jinsi ya kusimamia kipindi cha mpito.

Habari nyingine zinasema, maandamano mapya yanayodai utawala wa kiraia yameanza huko Khartoum, mji mkuu wa Sudan na miji mingine. Waandamanaji walimekusanyika katika kituo cha basi chenye pilikapilika nyingi zaidi kabla ya kuandamana kuelekea atika ikulu ya Republican.

Polisi wya Khartoum mapema ya siku hiyo waliimetangaza kufunga madaraja yanayounganisha miji mikuu mitatu ya Khartoum, Omdurman na Bahri, ambako na askari wamepelekwa kulinda atika ma ilango ya madaraja hayo.