Rais Isaias Afeworki wa Eritrea amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi aliyefanya ziarani nchini humo.
Kwenye mazungumzo yao Rais Afeworki amesema, urafiki kati ya Eritrea na China una msingi imara, na Eritrea siku zote inaunga mkono kithabiti China kulinda mamlaka na uhuru wake, na kuheshimu msimamo halali wa China. Amesema Eritrea imeweka mpango wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, inatarajia kujifunza kutokana na uzoefu wa maendeleo ya China na kuendeleza ushirikiano haswa kwenye sekta za miundombinu, raslimali za madini, kilimo na raslimali watu.
Eritrea ni kituo cha kwanza cha ziara ya kwanza ya Bw. Wang katika mwaka huu mpya, hali ambayo inaonesha kuwa China inatilia maanani uhusiano kati yake na Eritrea. Amesema wakuu wa nchi hizo mbili wameamua kupandisha uhusiano kati ya China na Eritrea kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati, na China inapenda kutumia fursa hii, kutekeleza ipasavyo makubaliano yaliyofikiwa kati ya wakuu wa nchi hizo mbili, na kusukuma mbele ushirikiano kati ya pande mbili ufikie kwenye ngazi mpya.
Siku hiyohiyo Bw. Wang Yi pia alikutana na mwenzake wa Eritrea Osman Saleh.