Watu watano wamekufa katika ajali ya radi magharibi mwa Tanzania
2022-01-06 09:00:10| CRI

Watu watano ikiwa ni pamoja na watoto wamekufa baada ya kupigwa radi mkoani Kigoma.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma Bw. James Manyama amesema watoto hao wanne walipigwa radi jumanne jioni katika kijiji cha Kibuye. Watoto hao waliokuwa wanacheza chini ya mwembe wanatoka katika familia tofauti. Mtu mwingine wa tano aliyekufa ni mkulima mwanamke aliyekuwa shambani jioni.

Polisi wamewataka wazazi na walezi kutoruhusu watoto wako kucheza chini ya miti wakati mvua zinaendelea, ili kuepusha kupigwa radi.