Waziri wa mambo ya nje wa China atembelea nchini Kenya
2022-01-06 09:18:23| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amewasili nchini Kenya na kuanza ziara rasmi ya siku mbili.

Ubalozi wa China nchini Kenya umesema ziara ya Bw. Wang Yi itafuatilia mambo mbalimbali, ikiwemo kuhimiza utekelezaji wa matokeo yaliyopatikana katika Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Novemba mwaka jana nchini Senegal, na kubadilishana maoni na upande wa Kenya kuhusu hatua mpya za kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Pia pande mbili zitazungumizia mahitaji ya misaada kwa Kenya ili kukabiliana na janga la virusi vya Corona na kufufua uchumi wake.

Ziara ya Bw. Wang Yi inatarajiwa kutoa fursa mpya ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi wa kina kati ya China na Kenya.