Rais Uhuru wa Kenya na Bw. Wang Yi kukagua maendeleo ya gati la mafuta la Kipevu
2022-01-06 09:00:48| CRI

Rais Uhuru Kenyatta na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo wanatarajia kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati la mafuta la Kipevu lililopo katika bandari ya Mombasa.

Gati hilo linalojengwa na Kampuni ya China linatarajiwa kuwa na eneo la kisiwa na sehemu nne zenye jumla ya urefu wa meta 770. Eneo hilo pia linaunganishwa na kituo cha kusafisha mafuta cha Kenya (KPRL) na shirika la kusafirisha mafuta Kenya (KPC).

Baada ya kukamilika gati zima litaweza kushughulikia mafuta ya aina mbalimbali, likiwa na uwezo wa kupokea kwa pamoja meli tatu zenye uzito wa tani laki 2, na kitachukua nafasi ya kituo cha zamani kilichojengwa mwaka 1963.