Msomi wa Mali: Mafanikio yaliyopatikana China mwaka 2021 ni somo kwa dunia
2022-01-06 10:04:24| CRI

Msomi wa Mali: Mafanikio yaliyopatikana China mwaka 2021 ni somo kwa dunia_fororder_Yoro2

Mtaalamu wa mambo ya kimataifa kutoka Mali na mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa nchi zinazotumia lugha ya Kifaransa cha Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Prof. Yoro Diallo amesema, hotuba ya mwaka mpya wa 2022 ya Rais Xi Jinping wa China imefanya majumuisho kuhusu mafanikio yaliyopatikana China katika mwaka 2021, ambayo ametaja kama somo kwa dunia nzima.

Akihojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Prof. Diallo amesema, Rais Xi Jinping aliyataja mafanikio ya China katika mwaka 2021 kuwa “yana maana kubwa”. Katika mwaka huo uliopita, China imekamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora, ilisherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China CPC, na kuanza safari mpya ya kuelekea miaka 100 ya pili. Profesa Diallo anaona ingawa mwaka 2021 janga la virusi vya Corona bado lilikuwa limeendelea duniani, lakini dunia imeshuhudia watu wa China wakiwa chini ya uongozi wa CPC walivyofuata kithabiti njia ya kuelekea ustawi mpya wa taifa la China.

Prof. Diallo amesikia moyo wa Rais Xi Jinping wa kuwajali wananchi kwenye salamu zake za mwaka mpya. Akimnukuu rais Xi ambaye alisema “kila mara ninapotembelea nyumba za wananchi, huwa ninawauliza wana matatizo gani maishani, na huwa nayaweka moyoni waliyoniambia”, “pia natoka kijijini, nina kumbukumbu binafsi kuhusu umaskini”...Prof. Diallo amesema maneno hayo ya kutia moyo yameonesha kuwa CPC na serikali ya China kweli wanayachukulia “matarajio ya wananchi kwa maisha bora” kuwa malengo yao, na hii pia ni sababu kwa CPC na serikali ya China kuungwa mkono kithabiti na wananchi wao.

Prof. Diallo amesema hotuba ya mwaka mpya ya Rais Xi pia imeonesha moyo wa China wa kujali na kukumbatia dunia. Kwenye hotuba yake, Rais Xi amesema China imetoa jumla ya dozi bilioni 2 za chanjo ya COVID-19 kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 120 duniani, mbali na hayo Rais Xi pia ameeleza dhamira ya China ya kuandaa vizuri michezo mingine ya Olimpiki. Prof. Diallo anaona kuwa, hatua za China za kutoa chanjo kwa nchi za nje na kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, zote zimeonesha uungaji mkono wa China kwa mfumo wa pande nyingine, na vilevile ni utekelezaji halisi wa dhana ya Jumuiya ya Binadamu yenye Hatma ya Pamoja.

Prof. Diallo amesema, mwaka 2022 ni mwaka wa chui katika utamaduni wa China, kama alivyoandika mwandishi wa Nigeria Wole Soyinka kuwa “Chui hajidai kwa nguvu yake, anafuata tu windo lake”, China pia itakuwa kama chui ambaye hasumbuliwi na mazingira ya nje, na kusonga mbele tu kwa hatua madhubuti kuelekea lengo la miaka 100 ya pili.