Spika wa bunge Tanzania ajiuzulu kutokana na tifu la madeni
2022-01-07 09:08:58| cri

Spika wa bunge Tanzania Job Ndugai amejiuzulu jana Alhamis kufuatia video aliyoikosoa serikali kwa mwenendo wake wa kukopa akisema sio mwenendo mzuri.

Kwenye taarifa iliyotolewa bungeni mjini Dodoma, Ndugai amesema amemuandikia barua katibu mkuu wa chama tawala cha CCM akimuelezea kuhusu kujiuzulu kwake. Pia amesema amejiuluzu kwasababu zake binafsi na kwa ajili ya kulinda maslahi mapana ya taifa, serikali na chama chake.

Jumatatu, Ndugai alimuomba radhi hadharani rais Samia Suluhu Hassan kufuatia kauli alizotoa mapema wiki iliyopita kwamba Tanzania inajiingiza kwenye hatari ya kupigwa mnada kutokana na kuongezeka kwa madeni ya taifa. Jumanne rais Samia alitupilia mbali kauli kwamba serikali inakopa akiwahakikishia watu kwamba uongozi wake unakopa kwa ajili ya maendeleo ya miundo mbinu.