China na Kenya kuimarisha na kupanua ushirikiano katika nyanja nne
2022-01-07 09:07:20| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema yeye na mwenzake wa Kenya Raychelle Omamo wamefikia makubaliano kwamba China na Kenya ziimarishe uhusiano wao katika nyanja nne.

Akitaja nyanja hizo Bw. Wang amesema kwanza nchi hizo mbili zinahitaji kuwa washirika ambao wanasaidiana kwa dhati, hasa katika kulinda mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi, kulinda haki halali na maslahi yao ya pamoja, na kutumia njia ya maendeleo inayofaa kwa hali ya nchi.

Pili nchi hizo mbili zinahitaji kushirikiana katika kuongeza kasi ya maendeleo na kujifufua. China na Kenya zitaendelea kuimarisha ushirikiano wa maendelo ya miundombinu, biashara na uwekezaji na kuisadia Kenya katika kuhimiza ukuaji wa viwanda na kuwa ya kisasa.

Mbali na hayo Bw. Wang pia ametaja nyanja ya tatu ni kuwa nchi zote mbili zinahitaji kuwa washirika katika kuhimiza umoja wa China na Afrika. Na nne ni kushirikiana kulinda amani ya kikanda.