Watu 58 wauawa katika mashambulizi kaskazini magharibi mwa Nigeria
2022-01-10 08:34:37| cri

Watu zaidi ya 58 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wenye silaha katika vijiji kadhaa vya wilaya ya Anka na ya Bukuyum katika jimbo la Zamfara, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Msemaji wa gavana wa jimbo hilo Bw. Ibrahim Zaouma alisema, mashambulizi hayo yalitokea jumatano na alhamis wiki iliyopita, ambapo nyumba kadhaa pia zilichomwa moto.

Habari zinasema, Gavana wa jimbo hilo Bello Matavale ametembelea vijiji hivyo ili kujua hali halisi, na kuahidi kuwa serikali itachukua hatua kali kupambana na wapiganaji hao na kulinda usalama wa watu.