ECOWAS yaweka vikwazo vikali kwa Mali
2022-01-10 08:34:25| CRI

Uongozi wa Jumuiya ya Kiuchumu ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuweka vikwazo vikali dhidi ya Mali.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano wa viongozi wa Jumuiya hiyo mjini Accra, Ghana, imesema, utaratibu uliotolewa na mamlaka ya mpito nchini Mali unaoweka muda wa mpito kuwa miaka mitano na nusu haukubaliki, na nchi wanachama wa ECOWAS zitaondoa mabalozi wao nchini Mali.

Taarifa hiyo pia imesema, vikwazo vingine vilivyotangazwa ni kufunga mpaka wa ardhini na angani kati ya nchi wanachama wa ECOWAS na Mali, kusitisha biashara kati ya nchi hizo na Mali, isipokuwa kwa bidhaa muhimu za matumizi.