Baraza la utawala la Sudan launga mkono pendekezo la Umoja wa Mataifa la kumaliza mgogoro wa kisiasa
2022-01-11 08:35:32| CRI

Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan limepongeza pendekezo lililotolewa na Umoja wa Mataifa la kuwezesha majadiliano ya kina kati ya pande husika nchini humo ili kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Baraza hilo limeweka wazi msimamo wake wakati wa mkutano uliofanyika Ikulu na kuongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan. Baraza hilo limetoa wito wa kujumuisha Umoja wa Afrika kuunga mkono pendekezo hilo na kuchangia mafanikio ya majadiliano nchini humo.

Pia Baraza hilo limesisitiza haja ya kuongeza kasi ya kuunda serikali ya mpito kuondoa pengo lililoachwa wazi baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abdalla Hamdok kujiuzulu Januari 2 mwaka huu.