Mtu mmoja auawa na wengine 30 wajeruhiwa katika maandamano nchini Sudan
2022-01-11 08:36:44| CRI

Mtu mmoja auawa na wengine 30 wajeruhiwa katika maandamano nchini Sudan_fororder_VCG31N1237623634

Jeshi la Polisi nchini Sudan limesema mtu mmoja ameuawa na wengine 30 kujeruhiwa, wakiwemo raia na askari polisi, wakati wa maandamano makubwa yaliyofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na miji mingine jumapili.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi hilo imesema, askari polisi 22 walijeruhiwa katika maandamano hayo, na polisi walitumia nguvu kidogo kushughulika na waandamanaji hao. Pia Jeshi hilo limesema, wakati wa maandamano hayo, watu 86 walikamatwa na hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi yao.

Maelfu ya Wasudan waliandamana siku ya jumapili katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum na miji mingine wakidai utawala wa kiraia, licha ya juhudi za pande husika za kuleta suluhisho la kisiasa la mgogoro huo.