Watu watatu wauawa katika mlipuko mashariki mwa Tanzania
2022-01-12 08:17:46| cri

Polisi nchini Tanzania wamesema watu watatu wamefariki kufuatia mlipuko uliosababishwa na kitu kinachoshukiwa kuwa ni guruneti katika kijiji cha Pongwe Msungura mkoani Pwani, nchini humo.

Kamanda wa polisi wa Pwani Bw. Wankyo Nyigesa amesema, watu hao waliokota kitu walichoshuku kuwa ni guruneti ambacho kilililipuka wakati wakikichunguza na kusababisha vifo hivyo.

Amesema polisi walikusanya mabaki ya bomu hilo kwa uchunguzi zaidi utakaothibitisha kama kifaa hicho ni guruneti.