Huawei yaisaidia Zambia kuingia kwenye “zama ya 5G”
2022-01-12 08:19:15| cri

 

   

Kampuni ya uendeshaji wa mawasiliano ya simu ya mkononi ya Zambia MTN kwa kushirikiana na kampuni ya Huawei ya China, imezindua rasmi mtandao wa 5G, na kuifanya Zambia kuwa nchi iliyo na mtandao wa 5G mapema barani Afrika.

Waziri wa sayansi na teknolojia wa Zambia Felix Mutati amesema, mtandao wa 5G ni zawadi ya mwaka mpya ya wananchi wa Zambia, na kutokana na ushirikiano na kampuni ya Huawei, Zambia imekuwa moja ya nchi kumi zilizo na mtandao wa 5G mapema barani Afrika.

Hatua hiyo imeboresha zaidi kiwango cha miundombinu ya mawasiliano na upashanaji wa habari nchini humo, na kuweka msingi imara kwa mpango wa kidigitali unaoendelea kutekelezwa.