Rais wa Somalia aunga mkono makubaliano kuhusu uchaguzi
2022-01-12 08:19:45| CRI

Rais wa Somalia aunga mkono makubaliano kuhusu uchaguzi_fororder_Farmajo索马里总统

Rais Mohamed Farmajo wa Somalia amepongeza maafikiano yaliyofikiwa jumapili na viongozi wa kisiasa nchini humo, na kutoa wito kwa pande husika kuongeza kasi ya utekelezaji wa ratiba iliyokubalika ya uchaguzi.

Akihutubia wananchi kwa kupitia televisheni kuhusu hali ya sasa nchini humo, rais Farmajo alieleza matumaini yake kuwa uchaguzi wa Bunge la Chini na urais utafanyika katika mazingira ya amani. Amesema yuko tayari kwa uchaguzi kufanyika baadaye mwaka huku, na kusisitiza kuwa mchakato wa uchaguzi lazima uongozwe na Wasomali wenyewe.

Kauli hiyo ya rais Farmajo imekuja siku moja baada ya waziri mkuu wa Somalia na viongozi sita wa kikanda kufikia makubaliano kuhusu kumaliza uchaguzi wa bunge itakapofika Februari 25, na njia za kuboresha usalama wa Ikulu.