SADC yaeleza umuhimu wa amani na usalama kaskazini mwa Msumbiji
2022-01-13 08:30:47| CRI

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeleeza umuhimu kwa nchi wanachama kuimarisha jukumu la kikanda katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, mpaka amani itakapopatikana.

Azimio hilo limefikiwa katika mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC waliokutana mjini Lilongwe, Malawi, jana jumatano, kutathmini Tume ya Dharura ya SADC nchini Msumbiji (SAMIM).

Akizungumza katika mkutano huo, rais wa Malawi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Lazarus Chakwera, amesema vikosi vya Tume hiyo kwa kushirikiana na jeshi la ulinzi la Msumbiji na wenzi wengine wamerejesha matumaini kwa wakazi wa Cabo Delgado. Amezitaka nchi wanachama kuendelea kuungana dhidi ya vitendo vya kigaidi hususan katika mkoa huo, na kwenye kanda hiyo, na kuzikaka kuongeza lengo la kutimiza Amani katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji.