Rais wa Zimbabwe aishukuru China kwa msaada wa chanjo ya COVID-19
2022-01-13 08:38:37| cri

 

 

Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe jana ametoa hotuba kupitia televisheni ambapo ameishukuru serikali ya China kwa msaada wa chanjo ya COVID-19.

Amesema Zimbabwe inakabiliwa na wimbi la nne la COVID-19, pia inapambana na virusi vya Omicron, na msaada huo wa China utasaidia mapambano dhidi ya janga hilo.

Rais Mnangagwa amesema msaada wa chanjo kwa Zimbabwe umeonesha utimizaji wa ahadi wa China, na kupitia msaada huo, nchi nyingi za Afrika ikiwemo Zimbabwe na nchi nyingine zinazoendelea zimepata chanjo kwa gharama nafuu na zenye ufanisi.

Rais Mnangagwa pia amesema, licha ya msaada wa chanjo, China pia imetoa msaada wa vifaa vingi vya matibabu, na kutuma kikundi cha wataalamu wa matibabu nchini Zimbabwe ili kuisaidia kupambana na janga hilo.