Mali yaipongeza China kwa kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2022
2022-01-13 08:40:34| CRI

Msemaji wa serikali ya mpito ya Mali Abdoulaye Maiga amesema, nchi hiyo inaipongeza China kwa kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2022,

Kwenye taarifa yake, Maiga amesema, michezo hiyo inafanyika katika mazingira magumu ya kiafya kutokana na janga la COVID-19, hata hivyo, Michezo hiyo itaimarisha urafiki na undugu kati ya mataifa kwa mujibu wa moyo wa Olimpiki, na haipaswi kuingiliwa na masuala ya kisiasa.

Michezo ya Majira ya Baridi ya Olimpiki ya Beijing ya mwaka 2022 itafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 20 Februari.