Marekani yapaswa kufunga magereza yake ya siri kote duniani
2022-01-13 08:20:22| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana amesema, gereza la Guantanamo ni ukurasa mweusi katika historia ya haki za binadamu duniani, na Marekani inapaswa kufunga mara moja gereza hilo na magereza yake mengine ya siri kote duniani.

Bw. Wang Wenbin ameongeza kuwa, magereza hayo yanawakumbusha watu vitendo vibaya na uhalifu wa Marekani katika haki za binadamu. Kikundi cha wataalamu kutoka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kimetoa taarifa ikiilaani Marekani kwa kuendelea kutumia gereza la Guantanamo ambalo linakiuka haki za binadamu, na kusema kuwa kitendo cha Marekani cha kufunga na kunyanyasa watu wasiohukumiwa hakikubaliki.

Tarehe 11 Januari mwaka 2022 imetimiza mwaka wa 20 tangu gereza la Guantanao kuanzishwa.