Wimbi la nne la COVID-19 barani Afrika laelekea kupungua
2022-01-14 08:17:57| CRI

Wimbi la nne la COVID-19 barani Afrika laelekea kupungua_fororder_6

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika jana imetoa taarifa ikisema, wimbi la nne la maambukizi ya COVID-19 barani humo limepungua, lakini kiwango cha utoaji wa chanjo ya COVID-19 barani Afrika kimeendelea kuwa chini, hivyo nchi mbalimbali za Afrika zinapaswa kuharakisha zoezi la kutoa chanjo.

Taarifa hiyo imesema, katika kipindi cha wiki moja mpaka kufikia Januari 9, kesi za maambukizi ya COVID-19 barani Afrika zimepungua, na kiasi hicho katika eneo la kusini mwa Afrika kimepungua kwa asilimia 14 kuliko wiki iliyopita. Kesi za maambukizi ya virusi vya Omicron nchini Afrika Kusini zimepungua kwa asilimia 9 kuliko wiki iliyopita, na kesi hizo katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati pia imepungua. Lakini kesi katika Afrika ya Magharibi na Afrika ya Kaskazini zinaendelea kuongezeka.

Taarifa hiyo pia inasema, ni asilimia 10 tu ya watu barani Afrika wamepewa chanjo. Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti amesisitiza tena umuhimu wa kupata chanjo, na kuzitaka nchi mbalimbali za Afrika ziharakishe zoezi la kutoa chanjo ili kuokoa maisha ya watu wengi zaidi