Brigedia wa jeshi la polisi nchini Sudan auawa katika maandamano
2022-01-14 08:08:59| CRI

Brigedia Jenerali Ali Barima Hammad wa Jeshi la Polisi la Sudan ameuawa wakati wa maandamano ya kudai utawala wa kiraia yaliyofanyika jana katika mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.

Taarifa iliyotolewa jeshi hilo imesema, Brigedia Jenerali huyo aliuawa wakati akitimiza majukumu yake ya kuwalinda waandmanaji karibu na Maabara ya Tiba ya Stack.

Hata hivyo taarifa hiyo haikuweka wazi mazingira yaliyosababisha kifo cha polisi huyo mwandamizi, lakini mauaji hayo huenda yakaashiria kuongezeka kwa mapigano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama.