Kenya yazindua mfumo wa WRS ili kuhimiza usalama wa chakula
2022-01-14 09:22:36| cri

 

 

    Kenya jana imezindua jukwaa la kielektroniki litakalohimiza usalama wa chakula.

Waziri wa Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Ushirika nchini humo, Peter Munya amesema, Mfumo wa Stakabadhi za Ghala (WRS) utawawezesha wakulima na wafanyabiashara wa bidhaa za kilimo kuhifadhi mazao yao ili kupata stakabadhi za ghala (WR), ambazo zinaweza kufanyiwa biashara, kuuzwa, kubadilishana au kutumika kupata mikopo na pembejeo.

Bw. Munya amesema matumizi ya mfumo huo yanatarajiwa kupunguza hasara baada ya mavuno kutoka asilimia 40 hadi asilimia 10.