Rais wa Zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keita afariki dunia
2022-01-17 10:52:26| CRI

Rais wa Zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keita afariki dunia_fororder_马里

Rais wa zamani wa Mali Ibrahim Boubacar Keita amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76 Jumapili hii huko Bamako, mji mkuu wa Mali. Chanzo cha karibu na familia yake ndio kimetangaza msiba huu lakini hakikueleza sababu ya kifo chake.

Baada ya kuingia madarakani Septemba mwaka 2013 na kuchaguliwa tena mwaka 2018, Keita alipinduliwa Agosti 18 mwaka 2020, na Kamati ya kitaifa ya Wokovu wa Watu CNSP baada ya maandamano ya kupinga utawala wake yaliyoendelea kwa miezi kadhaa.

Muda mfupi baada ya mapinduzi hayo ya kisasa, mamlaka ya kijeshi ilimpa mafao yote kama anayopewa rais wa zamani wa Mali.

Tangu alipoondolewa madarakani, Keita alikaa mara kadhaa huko Dubai na Falme za Kiarabu, kutokana na sababu za kiafya.