13 wafariki na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali ya gari nchini Angola
2022-01-17 10:49:53| CRI

Watu 13 wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyotokea jana Jumapili katika jimbo la Huambo nchini Angola baada ya ya magari mawili kugongana.

Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi ya Taifa huko Huambo, Martinho Kavita Satito, sababu ya ajali hiyo ni mwendo kasi na uzembe wa madereva wa magari yote mawili. Ajali hiyo ilitokea saa sita mchana baada ya gari la Toyota HiAce na Kia Tourer kugongana uso kwa uso kwenye barabara ya sehemu ya Ussoque/Londoimbali. Baada ya kugongana Toyota HiAce iliungua moto na kusababisha watu 12 kufariki papo hapo na mmoja kufariki akiwa njiani wakati anapelekwa hospitali. Msemaji wa polisi amewataka madereva kuacha uzembe ili kuepuka ajali mbaya kama hiyo.