Somalia yafanya uchunguzi wa mashambulizi dhidi ya minara ya mawasiliano ya simu eneo la kusini
2022-01-17 10:53:45| CRI

Somalia yafanya uchunguzi wa mashambulizi dhidi ya minara ya mawasiliano ya simu eneo la kusini_fororder_索马里头图

Serikali ya Somalia imesema imeanza uchunguzi kuhusu mashambulizi ya anga yaliyotokea hivi karibuni ambayo yameteketeza minara ya mawasiliano ya simu na kudhoofisha shughuli za Kampuni mawasiliano ya simu ya Hormuud Telecom, ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano nchini humo.

Wizara ya Ulinzi imelaani mashambulizi hayo yaliyotokea huko Jubba na Gedi ambayo yalitekelezwa Jumanne katika eneo la Jilib ambalo ni ngome ya kundi la al-Shabaab katika eneo la Juba ya Kati. Hali halisi ya mashambulizi hayo bado haijajulikana.

Wizara hiyo imesema inawasiliana moja kwa moja na Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM na washirika wengine wanaotoa msaada kwa serikali hiyo katika operesheni za usalama ili kueleza wasiwasi wake na kujua kilichotokea katika maeneo hayo.