Mwakilishi wa China wa UM: Hatua ya ICC yapaswa kuhimiza utulivu na amani ya muda mrefu huko Darfur, Sudan
2022-01-18 10:22:50| CRI

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Geng Shuang ameeleza matumaini yake kuwa hatua ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai ICC inapaswa kusaidia kuhimiza utulivu na amani ya muda mrefu huko Darfur, Sudan.

China imekuwa ikifuatilia kwa karibu wakati ICC inashughulikia hali nchini Sudan, na imeona kazi iliyotekelezwa na mwendesha mashtaka wa ICC Karim Khan tangu aingie madarakani.

Baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Amani wa Juba, Darfur imeingia katika kipindi kipya cha ujenzi wa amani. China inazihimiza pande zote zilizosaini mkataba huo kuendelea na utekelezaji wa makubaliano ya amani na kutoa wito kwa makundi ambayo bado hayajatia saini kujiunga na mchakato wa amani haraka iwezekanavyo.