Uganda yaanza kutoa chanjo za nyongeza za COVID-19
2022-01-18 10:24:14| CRI

Uganda yaanza kutoa chanjo za nyongeza za COVID-19_fororder_乌干达

Uganda imeanza kutoa chanjo za nyongeza za COVID-19 kwa watu wanaopewa kipaumbele wakati nchi hiyo ikikabiliana na ongezeko la maambukizi.

Msemaji wa Wizara ya Afya ya nchi hiyo Emmanuel Ainebyoona amesema, watu wanaopewa kipaumbele ni pamoja na wenye umri wa miaka 50 na zaidi, wafanyakazi wa afya, walimu, viongozi wa kidini na utamaduni, wanausalama, watu wanaoshughulikia vyombo vya habari, madereva na wauzaji tiketi za magari ya umma. Wengine ni kama vile waendesha bodaboda, wafanyakazi wa baa na klabu za usiku, wafanyakazi na wachuuzi wa sokoni.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda mwenye umri wa miaka 77, amepewa dozi yake ya nyongeza mapema mwezi huu, akiwataka wananchi haswa wale wenye umri wa zaidi ya miaka 50, kupata chanjo ya nyongeza ili kujikinga dhidi ya athari mbaya za COVID-19.