FAO kutafuta fedha za kusaidia watu walio katika mazingira magumu katika Pembe ya Afrika
2022-01-18 10:25:38| CRI

FAO kutafuta fedha za kusaidia watu walio katika mazingira magumu katika Pembe ya Afrika_fororder_头图干旱

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema linahitaji kiasi cha dola za kimarekani milioni 138 kama ufadhili wa haraka ili kusaidia watu milioni 1.5 walio katika mazingira magumu katika nchi za Pembe ya Afrika ambapo mashamba na malisho yake yameathiriwa sana na ukame wa muda mrefu.

FAO ilitoa wito wa msaada mbalimbali kwa ajili ya kilimo nchini Ethiopia, Kenya na Somalia.

Mpango wa Kukabiliana na Ukame wa Pembe ya Afrika uliotolewa na FAO umetoa wito wa kutolewa zaidi ya dola milioni 138 ili kusaidia jamii za vijijini kuhimili tishio hili la hivi karibuni, ambapo dola milioni 130 kati ya hizo zinahitajika haraka kufikia mwisho wa Februari ili kutoa msaada wa muda kwa jamii zinazoishi kwenye mazingira magumu na zinazotegemea kilimo katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi.