Kenya yapanga kuiuzia China maparachichi
2022-01-19 09:39:16| CRI

Kenya yapanga kuiuzia China maparachichi_fororder_牛油果 头图

Afisa mkuu mtendaji wa mamlaka ya mazao mabichi ya Kenya FPC Okisegere Ojepat amesema, Kenya itaanza kuiuzia China maparachichi wakati biashara kati ya nchi hizo mbili ikiongezeka. 

Ojepat amesema hivi sasa majadiliano yanaendelea ili kuidhinisha mauzo ya maparachichi nchini China.

Ameeleza kuwa Huduma ya Ukaguzi wa Afya ya Mimea ya Kenya na wenzao wa China wanatarajiwa kufanya ukaguzi na kushughulikia masuala ya kiufundi, ili kuhakikisha kuwa maparachichi yanayopangwa kuuzwa yanafikia viwango vya ubora na usalama.

Pia ameongeza kuwa sasa wanauza maparachichi yaliyogandishwa katika soko la China, na makubaliano hayo mapya yanakaribishwa zaidi kwani yataongeza mapato ya mauzo ya ng’ambo ya nchi hiyo.