Watu wasiopungua sita wauawa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga nchini Somalia
2022-01-19 09:39:55| CRI

Watu wasiopungua sita waliuawa na wengine kumi kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu Jumanne jioni.

Polisi walisema mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliyevalia mkanda wa vilipuzi kiunoni alijilipua katika mgahawa ulioko karibu na kambi ya mafunzo ya kijeshi katika mji huo usio na utulivu.

Mashuhuda walisema shughuli za uokoaji zinaendelea pamoja na kuwakimbiza majeruhi hospitalini, na kuongeza kuwa mlipuko huo ulipasua paa la mgahawa huo.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.