Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa kukomesha vurugu nchini Sudan
2022-01-19 09:38:01| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kukomesha vurugu nchini Sudan ili kuruhusu juhudi za upatanishi.

Akiongea wakati alipoulizwa juu ya maoni ya katibu mkuu kuhusu vurugu za Sudan, msemaji wake Stephane Dujarric amesema wanalaani matumizi ya risasi na silaha za kuua dhidi ya waandamaji. Aidha amesema wanaendelea kuzitaka mamlaka kuruhusu watu kujieleza kwa amani, na waandamanaji wanapaswa kuandamana kwa amani. Na vikosi vya usalama vinapaswa kuwepo kwa ajili ya kulinda haki za watu za kuandamana kwa amani.

Wakati huohuo Bw. Dujarric amesema UM unajitahidi kupata ruhusa kwa ndege zake nchini Mali, wakati mamlaka zimeweka sheria mpya. Amesema hivi sasa ndege zote zimezuiliwa wakati wakiendelea kutafuta ruhusa kutokana na sheria mpya. Kwasababu wanafanya iwe ngumu kwa UM kutimiza jukumu lao.