Idadi ya watalii wanaofika Kenya yaongezeka kwa asilimia 53 mwaka 2021
2022-01-20 10:02:58| CRI

Idadi ya watalii wanaofika Kenya yaongezeka kwa asilimia 53 mwaka 2021_fororder_3

Waziri wa utalii na wanyamapori wa Kenya Bw. Najib Balala jana alisema idadi ya watalii wanaofika Kenya imefikia 870,465 katika mwaka 2021, idadi ambayo imeongezeka kwa asilimia 53 ikilinganishwa na 567,848 ya mwaka 2020, hali ambayo imeonyesha ufufukaji wa sekta ya utalii kwenye kipindi cha janga la Corona baada ya kuongeza utolewaji wa chanjo ya COVID-19 duniani.

Amesema sekta ya utalii ya Kenya imeendelea kukua kwa utulivu kuanzia mwezi Juni hadi Disemba katika mwaka 2021. Ingawa idadi hiyo ni ndogo, lakini inatarajiwa kurejea kama ya zamani au hata kuizidi. Ameongeza kuwa hali hiyo inatokana na wananchi wengi kupata chanjo ya Corona, hali ambayo inawafanya watalii wa kimataifa watake tena kufika Kenya. Zaidi ya hayo, jitihada za soko la utalii, imani ya kushinda mapambano dhidi ya janga la Corona, bidhaa za uvumbuzi zilizotolewa na hoteli na mashirika ya ndege ya ndani pia zinachangia ongezeko hilo.