Sinovac kuipatia Misri vifaa vya baridi kwa ajili ya kuhifadhi chanjo
2022-01-20 10:01:48| CRI

Ubalozi wa China nchini Misri umesema, Kampuni ya Sinovac imesaini makubaliano ya ushirikiano na Kampuni ya Holding ya Misri inayoshughulikia Bidhaa za Kibaiolojia na Chanjo (VACSERA) ili kuweka vifaa vya baridi kwa ajili ya kuhifadhi na kutunza chanjo nchini Misri.

Makubaliano hayo yamesainiwa na makampuni hayo mawili kwa njia ya video na baadaye kufanyika hafla nje ya mtandao wa internet iliyohudhuriwa na Kaimu Waziri wa Afya na Elimu ya Juu wa Misri Khaled Abdel-Ghaffar na Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang kwenye makao makuu ya Wizara ya Afya huko Cairo. Balozi wa China amesema ushirikiano wa kupambana na janga kati ya China na Misri umeendelea kuwa wa kina na ushirikiano wa chanjo umeshuhudiwa ukileta manufaa makubwa. Amesisitiza kuwa China iko tayari kuendelea kushirikiana na Misri katika kuzidi kuaminiana na kuondokana na ugumu kwa pamoja.

Naye Bw. Abdel-Ghaffar ametoa shukrani zake kwa usaidizi mkubwa wa China nchini Misri akisema wanatarajia kitengo cha baridi na mamilioni ya dozi za chanjo.