Mkuu wa UM atiwa moyo na matarajio ya amani nchini Ethiopia
2022-01-20 10:00:28| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jana alitiwa moyo na matarajio ya makubaliano ya amani katika eneo lenye mapigano kaskazini mwa Ethiopia.

Kwenye taarifa, Guterres amesema alikuwa na mazungumzo ya simu na mwakilishi mkuu wa Umoja wa Afrika katika pembe ya Afrika Olusegun Obasanjo, na kubadilishana naye mawazo kuhusu mgogoro wa Ethiopia baada ya ziara yake ya hivi karibuni huko Addis Ababa na Makelle mji mkuu wa mkoa wa Tigray.

Obasanjo amemtaarifu kuhusu juhudi zilizofanywa na serikali ya Ethiopia na Kundi la Ukombozi wa Watu la Tigray TPLF, za kuelekea kwenye ufumbuzi wa mgogoro. Bw. Guterres amesema Obasanjo ana imani kwamba sasa kuna fursa halisi ya ufumbuzi wa kisiasa na kidiplomasia juu ya mgogoro huo.