Tanzania yapanga kufuatilia wagonjwa laki 2 wa Ukimwi wasioandikishwa ili kudhibiti maambukizi mapya
2022-01-21 10:24:37| CRI

Tanzania yapanga kufuatilia wagonjwa laki 2 wa Ukimwi wasioandikishwa ili kudhibiti maambukizi mapya_fororder_2

Wizara ya Afya ya Tanzania imesema mipango inaendelea ya kuwafuatilia karibu watu laki 2 ambao ni wagonjwa wa Ukimwi wasioandikishwa ili kudhibiti maambukizi mapya.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema hivi sasa Tanzania ina wagonjwa wa Ukimwi milioni 1.7 lakini ni milioni 1.5 tu ndio wameandikishwa, na kuacha wengine laki 2 wakiwa hawajaandikishwa. Amesema wagonjwa hao wanaweza kufuatiliwa kupitia vipimo vinavyopaswa kufanywa kwenye ngazi ya vijiji, kata hadi wilaya, na kuongeza kuwa serikali inakusudia kutokomeza Ukimwi hadi kufikia mwaka 2030.

Mwalimu amesema asilimia 98 ya wagonjwa wa Ukimwi milioni 1.5 walioandikishwa wanaendelea kutumia dawa za ARV ambazo zinadhibiti Ukimwi na kulinda mfumo wa kinga ili mgonjwa aendelee kuwa na afya njema na kuishi muda mrefu.