Baraza la mpito la Sudan lakubali kuunda serikali inayoongozwa na waziri mkuu wa kiraia
2022-01-21 10:27:03| CRI

Baraza la mpito la Sudan linaloongozwa na jeshi la nchi hiyo limekubali kuunda serikali inayoongozwa na waziri mkuu wa kiraia ili kukamilisha majukumu ya kipindi cha mpito kinachoendelea.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Abdel Fattah Al-Burhan alieleza wazi msimamo huo wakati alipokutana na ujumbe wa Marekani unaoongozwa na msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Molly Phee na mjumbe maalumu wa Pembe ya Afrika David Satterfield katika Ikulu ya nchi hiyo.

Baraza hilo limeeleza kuwa liko tayari kufanya marekebisho ya kikatiba ili kuendana na maendeleo mapya ya uendeshaji wa uchaguzi huru na wa haki nchini Sudan ifikapo mwisho wa kipindi cha mpito.

Sudan na Marekani zilisisitiza kujumuisha vyama vyote vya Sudan katika mazungumzo ya kitaifa yanayoshirikisha makundi yote ya kisiasa na ya kijamii, isipokuwa chama cha National Congress Party kilichovunjwa, ili kufikia makubaliano ya kitaifa.