Ethiopia yapokea dozi milioni 2.2 za chanjo za ziada za Corona zilizotolewa na China
2022-01-21 10:19:23| CRI

Ethiopia yapokea dozi milioni 2.2 za chanjo za ziada za Corona zilizotolewa na China_fororder_头图

Serikali ya China jana ilichangia dozi milioni 2.2 za chanjo za ziada za Corona kwa Ethiopia, ili kuisaidia nchi hiyo katika kazi ya utoaji wa chanjo.

Kwenye hafla ya kukabidhi chanjo hizo, waziri wa afya wa Ethiopia Bibi Lia Tadesse amesema chanjo za Corona zinazochangiwa na China zinaokoa uhai wa wananchi, kitendo ambacho kimekuwa sehemu muhimu katika kazi ya utoaji wa chanjo nchini humo. Amesisitiza kuwa licha ya msaada wa chanjo za Corona, serikali ya China pia imeipatia Ethiopia msaada kwenye sekta za kukinga, kutibu na kupima virusi vya Corona.

Kwa upande wake balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Zhao Zhiyuan amesema msaada huo wa chanjo za Corona unafanya kazi muhimu kwenye mapambano dhidi ya janga la Corona nchini Ethiopia. China inathamini urafiki kati ya nchi hizo mbili, na itaendelea kuiunga mkono Ethiopia katika kupambana na virusi vya Corona.