Watu wasiopungua 20 wafariki dunia katika mlipuko uliotokea kwenye jamii ya wachimba madini nchini Ghana
2022-01-21 10:27:57| CRI

Takriban watu 20 walifariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye eneo la uchimbaji madini katika Mkoa wa Magharibi wa Ghana siku ya Alhamisi.

Seji Saji, naibu mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga, aliliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwamba mlipuko huo ulitokea katika eneo la Apiate baada ya lori lililokuwa limebeba vilipuzi vya kuchimba madini kugongana na pikipiki.

Pikipiki hiyo iliingia kwenye njia ya lori na kugongana nalo na kutoa cheche zilizosababisha mlipuko huo.

Afisa huyo alisema mlipuko huo ulikuwa na nguvu kubwa kiasi cha kuharibu takriban makazi 500 na kusababisha vifo vya watu wengi walio karibu.